Paul Makonda Apigwa Kombora Namba Mbili
WAKATI nchi ikiwa imelipuka na kumpigia kelele za kutaka Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, aoneshe cheti halisi cha kidato cha nne na kama hana
ajiuzulu, wapinzani wake hao wameibuka na kombora namba mbili ambalo ni
uraia wa mkewe, Ijumaa linakudadavulia. Awali, hoja ya vyeti feki
ilishikiwa bango zaidi na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na
Uzima la jijini Dar, Josephat Gwajima ambaye alisema ana ushahidi wa
cheti halisi cha Makonda chenye matokeo ya Divisheni 0 na kwamba
alitumia cha mtu anayeitwa Paul Christian Muyenge kilichomwezesha
kuendelea na msomo.
NI JUMAPILI ILIYOPITA Gwajima alitoa madai hayo mazito, Jumapili ya
Februari 26, mwaka huu, kwenye mahubiri ya ibada ya kanisani kwake,
Ubungo ambapo alisema kuwa, Makonda alitumia cheti hicho feki wakati
yeye alianza darasa la kwanza mwaka 1988, akitumia jina la Daudi Albert
Bashite.
MITANDAONI SASA Baada ya Gwajima kufunguka hayo, mitandao ya kijamii
ilianza ‘kumpiga’ Makonda kwa kumsema vibaya huku baadhi Chunguni
KIUJUMBE TOKA
Ukitaka ujue watu wanafahamu ulizaliwa wapi, unaitwa nani, ulisoma wapi,
ulifaulu vipi? Wachokoze ama chukua fomu kugombea chochote ndipo
utaelewa unaishi kwenye nyumba ya vioo! …Meseji Sent MAKONDA APIGWA…
wakimtaka aoneshe vyeti halali na kama hana, ajiuzulu au Rais Dk. John
Pombe Magufuli amtumbue.
WAZIDI KUMUANDAMA Kuna wengine walienda mbali zaidi, baada ya mkuu huyo
wa mkoa kwenda katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)
Usharika wa Kimara jijini Dar Jumapili iliyopita na kuangua kilio
alipokuwa ibadani, wakasema ‘hata akilia wao wanataka vyeti.’
“Hatutaki ulie, toa vyeti baba,” alichangia mmoja wa wafusi wa Mtandao
wa Facebook. KUSUDI LA MAKONDA Kwenye ibada hiyo, Makonda alipopewa
nafasi ya kuzungumza, alitumia mwanya huo kueleza namna ambavyo ameingia
kwenye vita kubwa ya madawa ya kulevya ambayo wengi waliowahi
kuianzisha walipoteza maisha ama walifungwa.
Alisema, inahitaji usimame na Mungu wa kweli ili uweze kufanikiwa
kuishinda vita ya madawa ya kulevya kwani wanaohusika, wana nguvu kubwa
ya kufanya lolote lakini yeye amejitoa mhanga kumsaidia Rais Magufuli
aliyemteua.
“Kwenye hii vita, kila aliyeingia ni ama aliuawa au alifungwa au
alipotezwa kwa namna yoyote ile,” alisikika Makonda akisema. Kuonesha
kwamba yupo tayari kwa lolote, Makonda alisema yeye haoni tatizo kuukosa
wadhifa wa ukuu wa mkoa kwa siku moja lakini hawezi kukubali katika
utawala wake, vizazi viangamie kwa madawa ya kulevya.
“Hata kama nitakuwa mkuu wa mkoa kwa siku moja lakini ilimradi nimetimiza kusudi la Mungu, nipo tayari,” alisema Makonda.
ALIGUSIA KOMBORA NO. 2 Katika mazungumzo yake kanisani hapo, Makonda
alionesha kunusa harufu ya kombora la pili ambalo ameandaliwa ili
kukwamisha jitihada zake za kupambana na madawa ya kulevya ukiacha lile
namba moja la vyeti ambalo ndilo lilikuwa ‘hot’.
“Baba mchungaji huwezi amini sasa hivi wametoka kwenye suala la vyeti,
wamehamia kwa mke wangu. Naye wanasema si raia,” alisema Makonda.
MITANDAO YAKAZIA SASA Baada ya Makonda kusikika hivyo, mitandao ilizidi
kuchochea moto suala hilo na kusema kwamba ni kweli mkewe si raia kwani
hata uso wake unaonesha.
“Wewe humuoni alivyo? Anaonekana kama raia wa kigeni hivi, wakimfuatilia
watajua na ninaamini ushahidi ni rahisi sana kupatikana. Vimepatikana
vyeti sembuse uraia, tutashuhudia mengi mwaka huu,” alichangia jamaa
aliyejiita Mehans mtandaoni.
MAKONDA AKESHA AKIMUOMBA MUNGU
Taarifa za ndani zimedai kuwa kutokana na makombora hayo, Makonda
ameamua kumshtakia Mungu na kumuacha ayashughulikie maana anaamini
dhamira yake ilikuwa njema katika mkoa na taifa lake. “Makonda sasa
anapambana kiimani, ameamua akeshe kwenye maombi. Anafanya maombi,
anaamini mwisho wa siku Mungu wake atamtetea. Mungu hawezi kukubali
aangamie.
Wanamsakama kwa maneno, wanasahau ni Makonda huyo aliyejitoa kinaga
ubaga kudhibiti mashoga. “Makonda huyohuyo alijitoa kudhibiti matumizi
ya shisha, alisimama kidete kuendesha zoezi la kusalimisha silaha ambalo
lilichangia kupunguza uhalifu ndani ya jiji.
“Watu wanajiweka pembeni na hoja ya msingi ya madawa ya kulevya ambayo
mheshimiwa amejitoa. Amethubutu kuwataja wahalifu wa madawa hayo
yanayowaangamiza vijana, wao wanang’ang’ania suala la vyeti na uraia wa
mkewe kweli? Mungu atampigania,” kilisema chanzo kilicho karibu na
Makonda.
MADAI MENGINE
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali ambazo hazijathibitishwa, zinadai kuwa,
kuna uwezekano mkuu huyo wa mkoa akawa amemuandikia barua rais kuomba
kujiuzulu ili kuondokana na ‘presha’ ya maadui wanaomsakama. Hata hivyo,
Makonda na ofisi ya rais, hawajazungumzia lolote kuhusiana na madai
hayo yaliyoenea.
KUTOKA KWA MHARIRI
Makombora anayorushiwa Makonda si jambo la ajabu sana kwani historia
inaonesha kuwa, wengi waliojaribu kugusa mambo yenye madhara kwa jamii
lakini yaliyo na faida kwa baadhi ya watu waliishia kupingwa na
kuzushiwa mambo ya ajabu.
Hata hivyo, makombora yote mawili aliyopigwa Makonda ni mepesi na anayo
nafasi ya kuyapangua yasimuathiri endapo ataamua kuweka kila kitu wazi
ili kuwaumbua wazushi wanaotaka kumharibia sifa yake nzuri. Kinyume
chake, sifa yake aliyojijengea kwa muda mrefu itakuwa imeingia doa.
Post a Comment