MAN UNITED, WAKIIWEZA HII BASIIIII WANATINGA TOP FOUR
WIKI
hii hakutakuwa na utamu wa Premier League. Mambo yote yataanza katika
wiki ya Aprili Mosi kuelekea safari ya mechi za mwisho kabisa.
Zitakuwa
ni tisa, kumi au 11 kulingana na timu zilivyocheza. Ubingwa nafasi
zaidi iko kwa Chelsea pia angalau Tottenham wanaonekana kuwa na mwendo
mzuri kama hawatateleza.
Manchester
United ilikuwa ikizungumziwa kwenye ubingwa kila ulipofikia wakati huu.
Lakini imepotea kwa takriban misimu minne mfululizo.
Msimu
huu inaonekana kuwa na nafuu kubwa ingawa mwanzoni ilibezwa. Kutoka
kuwa “mmiliki” wa nafasi ya saba, baadaye ya sita na sasa wako nafasi ya
tano wakiwa wanafukuzia kuingia nafasi ya Top Four.
Takriban
mwezi na nusu sasa, nilisema Man United wana nafasi kubwa ya kuingia
Top Four, zaidi nikichambua aina ya uchezaji wao, wanafunga mabao
machache lakini wagumu kupoteza.
Sasa
wana pointi 52 katika nafasi ya 5, Liverpool ina 56 ikiwa ndani ya Top
Four lakini utaona Man United wamecheza mechi 27 na Liverpool wana 29.
Kama
Man United itacheza mechi zote mbili na kushinda, maana yake itafikisha
pointi 58 na kuipiku Liverpool. Kama itakuwa hivyo basi kuna haja ya
kusema wakati wa kurejea Top Four utakuwa umewadia na inawezekana kutoka
itakuwa si kazi rahisi tena na unaweza kushangazwa nao ukisikia wako
katika nafasi ya pili.
Mechi
zao zinaweza kuwa mwamuzi mkubwa ingawa utaona sasa nafasi ya nne
katika Top Four inawaniwa na timu tatu ambazo ni Liverpool inayoshikilia
nafasi hiyo, Man United na Arsenal ambao wanaonekana kuwa ni
‘wataalamu’ wa nafasi hiyo ambao wako katika nafasi ya 6 wakiwa na
pointi 50, pia wakiwa wamecheza mechi 27.
Ukiangalia
kama Arsenal ni wa kuaminika, basi nao wakishinda mechi zao mbili,
watawafikia Liverpool. Hata wakiwa chini yao, wanaweza kuendesha presha
kuzidi kuwa kubwa lakini mwendo wao hauaminiki na si timu inayoweza
kupanga jambo na kulitekeleza kwa kutimiza ndoto.
Nilishawahi
kueleza kati ya Liverpool au Arsenal ni lazima moja iondoke kwenye Top
Four, wakati huo Tottenham ilionekana haina nafasi na Man City ilikuwa
ikiyumba ile mbaya. Sasa hali halisi inaanza kujitokeza.
Mechi
nne zijazo za Man United zitakazoanza Aprili Mosi hadi Aprili 15. Ni
siku za presha na mateso makubwa ya kutaka kubadili mambo lakini
zitakuwa mwamuzi sahihi wa nafasi ya Man United kurejea Top Four au la.
Man
itacheza dhidi ya Wes Brom, Everton, Sunderland na Chelsea. Inawezekana
kabla ya kuivaa Chelsea Aprili 15, ikawa imefikia mwafaka kuwa imerejea
au la na hakuna mechi laini lakini Man United wanaonekana kuanza
kujitambua kweli.
Kwa
Liverpool, huenda ndiyo wenye presha ya juu zaidi wakiwa na michezo
miwili zaidi na wana uhakika wa kushushwa nje ya Top Four kulingana na
hali halisi.
Mechi
zao nne kuanzia Aprili Mosi ni dhidi ya Everton, Bournemouth, Stoke
City na Wes Brom. Pia hakuna mechi laini hapa na utaona namna presha
itakavyozidi kupanda kwao hasa kama watakosea katika mechi moja tu.
Unaweza
kuona kama Arsenal nao wana nafasi kubwa lakini shida ni kuwa
hawaaminiki, kwamba wana uwezo hata wa kushinda mechi nne mfululizo.
Wakiweza hivyo, huenda wakatibua plani ya Man United na Liverpool.
Mechi
zao ni ngumu pia, ndani yake wanakutana na moja ya timu zilizo Top Four
ambayo ni Man City halafu West Ham, Crystal Palace na Middlesbrough,
nyingi zikiwa ni zenye presha ambazo hucheza kwa kujituma kweli.
Zitakuwa
ni siku 15 za presha na mwamuzi wa kile nilichokisema. Mechi hizo ndizo
zitatoa picha ya mwisho kuhusu Man United kuwa wanarejea Top Four au
wamefeli.
Man
United pekee ndiyo wamekuwa wakipanda lakini kwa Arsenal na Liverpool
kwa mujibu wa msimamo, wamekuwa wakiporomoka kila siku zinavyosonga
mbele. Man United wakishikilia hivyo, maana yake wana uhakika wa kuingia
Top Four na kumiliki nafasi moja.
Post a Comment