Kimenuka CCM: Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama, Emmanuel Nchimbi Kapewa Onyo Kali
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wanawake wa CCM taifa ambaye pia ni mbunge wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Sophia Simba na wenyeviti wa CCM wa
mikoa minne wamefukuzwa uanachama wa chama hicho kwa madai ya ukiukwaji
wa maadili ya chama
Mbali na maamuzi hayo, chama hicho pia kimewafukuza uanachama wenyeviti wanne wa mikoa ambao ni pamoja na Ramadhan Madabida (Dar es Salaam), Jesca Msambatavangu (Iringa), Erasto Kwilasa na Christopher Sanya (Mara).
Pia
chama hicho kimetangaza kuwavua uanachama wenyeviti wake katika wilaya
za Gairo, Babati Mjini, Kinondoni na Longido huku wengine wakipewa onyo
kali huku.
Panga
hilo pia limefika katika wajumbe wa NEC ambapo ndugu Ali Hera Sumaye
kutoka Babati Mjini naye akifukuzwa uanachama na wengine kupewa onyo
kali.
Maamuzi
hayo yamefanywa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama
hicho (NEC) kilichokaa leo mjini Dodoma kuelekea mkutano mkuu maalum wa
chama hicho utakaofanyika kesho JUmapili ya Machi 12, 2017.
Akizungumza
na wanahabari mjini humo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho,
Humphrey Polepole ametaja maamuzi mengine kuwa ni kutoa onyo kali kwa
mjumbe wake wa Kamati Kuu, Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye ni balozi wa
Tanzania nchini Brazil, huku Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam
Kimbisa akisamehewa
"Ndugu
Kimbisa amesamehewa makosa baada ya kuomba radhi, kujirekebisha na
kuwaongoza vyema wana CCM mkoa wa Dodoma kupata ushindi wa uchaguzi
mkuu, Ndugu. Emmanuel Nchimbi amepewa onyo kali na anatakiwa kuomba
radhi wanachama na uongozi wa CCM, tunajua huyu ni Balozi wetu Brazil,
lakini ametakiwa afanye hivyo mara moja akiwa huko huko Brazil, na
taarifa yetu ataipata" Amesema Polepole
Polepole amesema maamuzi hayo ni ya mwisho, na hayatakuwa na nafasi ya kukatiwa rufaa katika ngazi yoyote ya chama hicho.
Post a Comment