Harmorapa Amchana Mose Iyobo Kwenye Interview ‘Nina Hela, Aje Nimwajiri Kama Dancer Wangu
Baada ya kuachia track mpya iliyojaa utata utata hivi, Harmorapa ameweka
kila kitu ‘clear’ kilichomfanya kuandika mistari ya kumdiss dancer wa
Diamond, Mose Iyobo.
Kupitia kipindi cha Fleva Plus kinachoruka hewani kupitia Sunrise Radio,
DJ Dix alimuuliza kuhusu chanzo cha kile kinachoendelea kati yake na
dancer huyo kutoka WCB.
Harmorapa hakuona noma na alijibu maswali yote aliyoulizwa. Sauti yake
iliskika ikisema kwamba Mose Iyobo aambiwe kwamba anahitaji dancer na
angetaka awe ni yeye. Aliongeza kuwa anatumia dollars kwahiyo ana uwezo
wa kumuajiri na kumlipa vizuri tu.
“Mwambie Mose Iyobo nahitaji dancer, yeah nahitaji dancer kwa sababu
naweza mimi, nahitaji dancer so naweza kumlipa kwa sababu Harmorapa ana
dollar na pia anatumia account ya dollar,” alisema.
Katika hatua nyingine, alipoulizwa ni kwa nini aliamua kumdiss jamaa
kwenye ngoma yake aliyomshirikisha Juma Nature ‘Kiboko Ya Mabishoo’,
alisema…”Yani hata mfano naianza ile ngoma nilivyoiandika na nini,
mwanzo haikuwa vile ila baada ya kuja kunianza mimi ndo pale nikapata
feelings sana nikajikuta naandika vitu ambavyo vinamdiss pia na yeye ili
nimjibu.”
Harmorapa anahisi Mose Iyobo alichokoza nyuki pale alipomfananisha na
nyani kwa hiyo kung’atwa ni kitu cha lazima. Katika hatua nyingine,
rapper huyo alipinga kinachoonekana kama ana nguvu nyingi kwa upande wa
‘publicity stunt’ kuliko muziki wake.
Hali kadhalika, amewataka mashabiki zake wawe tayari kupokea kazi zake kwa kuwa amejipanga vizuri kimuziki mwaka huu.
Post a Comment