GENK YA SAMATTA YASONGA ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE
KRC Genk ya Ubelgiji anayoichezea Mtanzania Mbwana Samatta imefuzu kucheza hatua ya robo fainali katika Europa League.
Genk imefuzu baada ya sare ya bao 1-1 katika mechi ya pili ya hatua ya 16 Bora, leo.
Katika mechi ya kwanza, ikiwa ugenini, Genk iliibabua Gent kwa mabao 5-2 ikiwa kwake. Samatta alitupia mawili.
Sare ya 1-1, maana yake Genk inakwenda robo fainali kwa jumla ya mabao 6-3.
Samara
alicheza kwa dakika zote 90 na Genk ilipata bao lake kupitia Timothy
Castagne katika dakika ya 20. Bao likadumu hadi mwisho wa kipindi cha
kwanza.
Kipindi cha pili ilikuwa ni vita nikuvute na Gent wakapata bao la kusawazisha katika dakika ya 84 kupitia Louis Vertstrate.
Post a Comment