Dr. Makongoro Mahanga Atoweka.....Polisi Waendelea Kumsaka
Aliyekuwa
Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk. Makongoro
Mahanga, anayesakwa na Jeshi la Polisi ametoweka nyumbani kwake.
Mahanga
anasakwa na polisi kutokana na amri ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam, iliyoamuru akamatwe kwa kushindwa kumlipa Kainerugaba Msemakweli
zaidi ya Sh milioni 11 za kesi ya madai aliyomshinda.
Mahakama
hiyo ilitoa amri ya kukamatwa Machi 7, mwaka huu na kutoa nyingine
mwishoni mwaka wiki ambapo alitakiwa kufikishwa mahakamani jana. Hata
hivyo hakupatikana.
“Makongoro
Mahanga hajaja mahakamani na nyumbani kwake hayupo, anaendelea
kutafutwa,” alisema Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu, Ruth Masambu.
Hadi
jana, Mahakama Kuu ilishatoa hati mbili kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Ilala, ikielekeza Mahanga akamatwe na kufikishwa mahakamani.
Msemakweli
ambaye ni mlalamikaji, alikabidhiwa hati hiyo na kutakiwa kumkabidhi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni, ili aweze kutekeleza
amri hiyo.
Hamduni alikiri kupokea hati hiyo na kusema mdaiwa hajapatikana hivyo wanaendelea kumtafuta.
Dk. Mahanga, anatakiwa kumlipa mwanaharakati huyo baada ya kesi aliyofungua ya kashfa dhidi yake kufutwa mahakamani.
Post a Comment