Wabunge wa upinzani Walivyosusa na kutoka nje kisa kukamatwa kwa Tundu Lissu
Wabunge
wote wa vyama vya upinzani waliokuwa bungeni katika kikao
kinachoendelea jioni hii wametoka nje ya Bunge, wakipinga wenzao
kufukuzwa bungeni pamoja na kitendo cha Mbunge Tundu Lissu kukamatwa.
Wabunge
waliokuwa wameamuliwa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge na Naibu Spika Dkt
Tulia Ackson ni pamoja na mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa Bunda
Mjini Ester Bulaya na Mbunge wa Serengeti Marwa Ryoba.
Wabunge
hao watatu wamedaiwa kupinga uamuzi wa Naibu Spika kuhusu muongozo
ulioombwa na mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, kuhusu utaratibu
uliotumika kumkamata mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Mara
baada ya Naibu Spika kutoa maamuzi ya kuwaondoa wabunge hao watatu
bungeni, ndipo wabunge wengine wa upinzani pia wakaamua kutoka kama
ishara ya kupinga maamuzi hayo, pia ikiwa ni ishara ya kupinga utaratibu
wa kukamatwa kwa mbunge Tundu Lissu.
Nje
ya ukumbi wa Bunge, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe , amesema
wamefikia hatua hiyo kuonesha kuwa uataratibu unaotumiwa kukamata
wabunge wakiwa bungeni siyo sahihi, na kwamba kesho wataendelea na vikao
vya bunge lakini mapambano yataendelea.
"Kesho
tunarudi bungeni, lakini mapambano yataendelea, tunataka kuonesha kuwa
utaratibu huu wa kuvizia wabunge kwenye milango ya bunge bila taarifa
rasmi ya Spika na bila kuwaeleza wabunge sababu za kukamatwa kwao siyo
sawa. Tukilifumbia macho litakuja kumtokea mbunge yoyote hata wa CCM" Amesema Zitto.
Post a Comment