SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA, MAKONDA AMTAJA MANJI, AMTAKA KUFIKA POLISI KUHOJIWA
Kutoka kushoto ni Manji, Gwajima, Azzan na Mbowe |
Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji ni mmoja wa watu maarufu waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar, kuwa wanahitajika keshokutwa Ijumaa kwenye kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na madawa ya kulevya.
Makonda ametaja orodha ya majina kadhaa marufu kati ya 65 aliyodai kuwa anayo katika orodha yake ya wanaotakiwa kufika kituoni hapo kwa ajili ya zoezi hilo la mahojiano katika kampeni yake ya kuendeleza kupambana na utumiaji na biashara ya madawa ya kulevya.
Manji |
Majina mengine maarufu yaliyopo katika orodha hiyo ni na mfanyabiashara maarufu wa nguo, Hussein Pambakali, Mbunge wa Hai, Freeman Aikaely Mbowe, Mchungaji Josephat Gwajima.
Paul Makonda |
Ameielezea orodha hiyo kuwa ni ya wale ambao wanahisishwa na biashara hiyo haramu na wengine wana taarifa muhimu zinazoweza kuwasaidia polisi kuwatia nguvuni vinara wa biashara hiyo.
Watu hao watahojiwa na polisi kama ilivyofanyika kwa watu waliotajwa kwenye orodha ya kwanza iliyohusisha pia mastaa wa muziki na filamu.
Wengine wanaohitaji ni pamoja na wamiliki wa Slipway na Yatchy Club.
Orodha ya awamu ya pili ya Makonda ina jumla ya majina 65.
Kusema kweli Manji amefanya mengi kwa jamii yetu Tanzania. Tupunguze makali wote sisi ni waathirika.
ReplyDelete