Maamuzi ya mahakama kuhusu wasanii wanaoshtakiwa kwa dawa za kulevya
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana imetoa maamuzi kwa
baadhi ya wasanii waliokuwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma
za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Mahakama
hiyo imekubali maombi ya Jamhuri kuhusu tuhuma zinazomkabili Petitman
na wenzake wanne kwamba watakuwa nje kwa dhamana ya shilingi milioni 20
na watatakiwa kuripoti kituo cha polisi mara mbili kwa mwezi kwa muda wa
miaka mitatu na kila mmoja anatakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwaminifu.
Aidha kwa TID, Tunda, Recho, Rommy Jones, Babu wa Kitaa na Nyandu Tozi watakuwa chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja na dhamana ya Tsh milioni 10, wakivunja masharti watarudi Mahakamani
Aidha kwa TID, Tunda, Recho, Rommy Jones, Babu wa Kitaa na Nyandu Tozi watakuwa chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja na dhamana ya Tsh milioni 10, wakivunja masharti watarudi Mahakamani
Post a Comment