Alichokisema Zitto Kabwe Bungeni Kuhusu Sakata la Wema Sepetu Kukamatwa na Madawa ya Kulevya
“Kamati
(ya Bunge) imelalamika kuwa Mamlaka ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya ina
bajeti finyu na hata hiyo bajeti haitolewi na hivyo kusababisha Mamlaka
kukosa vitendea kazi, kushindwa kutoa elimu kwa umma, kushindwa kufanya
operesheni za ukamataji wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya na
kushindwa kutoa ushauri nasaha kwa waathirika,” alisema Zitto.
Zitto
alikuwa akizungumzia taarifa ya Kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi
imebaini dosari nyingi katika sera ya dawa za kulevya ya mwaka 2004
ambayo imepitwa na wakati.
Wakichangia
katika taarifa ya shughuli za kamati kwa mwaka 2016/17, wabunge,
akiwemo Zitto, walisema dawa za kulevya ni janga la taifa na linahitaji
mikakati ya kupambana na siyo kuwaweka rumande waathirika ambao
wanahitaji kupatiwa matibabu.
Zitto
alibainisha kuwa watuhumiwa waliokamatwa katika vita inayoendelea
jijini Dar es Salaam wamelazwa ndani kwa zaidi ya siku tatu bila
kufikishwa mahakamani.
“Baadhi ya watuhumiwa wameelezwa kuteswa na kupigwa na polisi na kulazimishwa kutoa maelezo kwa Polisi," alisema Zitto. "Umma haujaelezwa kama watu hawa wamekamatwa na madawa hayo ama wamehisiwa kuwa ni watumiaji tu.”
Post a Comment