WACHEZAJI WA YANGA HAWAFURAHISHWI NA HAYA YA KOCHA LWANDAMINA
Imefahamika
kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina, ndiyo chanzo cha
kipigo cha mabao 4-0 walichokipata katika mchezo dhidi ya Azam FC.
Yanga
ilikutana na kipigo hicho juzi Jumamosi katika mechi ya mwisho ya
makundi kwenye Kombe la Mapinduzi iliyochezwa katika Uwanja wa Amaan,
Zanzibar.
Kipigo
hicho walichokipata Yanga, kimewaondoa kileleni kwenye msimamo wa Kundi
B, wakiwa na pointi 6 huku Azam wakiongoza wakiwa na 7.
Kwa
mujibu wa taarifa ambazo zimepatikana kutoka kwa wachezaji wa timu
hiyo, uchovu wa mazoezi magumu saa chache kabla ya mechi ndiyo sababu ya
wao kupoteza pambano hilo.
Mtoa
taarifa huyo alisema, timu hiyo siku ya mechi asubuhi walifanyishwa
mazoezi kama kawaida kwa muda wa saa mbili wakati usiku wakiwa na mechi.
Aliongeza
kuwa, katika mazoezi yao hayo, walifanya programu zote ikiwemo kukimbia
mbio fupi (short splint), mbio ndefu na kuruka koni kabla ya kumalizia
programu ya kupiga penalti, kitu ambacho siyo sahihi na badala yake
walitakiwa kupumzika kwa ajili ya kujiandaa na pambano hilo.
“Kiukweli
kabisa ilikuwa lazima tufungwe mechi na Azam, na hiyo imetokana na
wachezaji wote kuwa na uchovu na kama ulifuatilia mchezo ule, utaona
wachezaji wote tulikuwa tumechoka kutokana na mazoezi magumu tuliyofanya
asubuhi wakati jioni tukiwa na mechi ngumu.
“Kwa
mfano, mimi (jina kapuni), nilishindwa kutimiza majukumu yangu kutokana
na uchovu niliokuwa nao, kwa kweli kama tukiendelea na programu hii ya
siku ambayo tunacheza mechi jioni halafu tukafanya mazoezi asubuhi, basi
tutaendelea kufungwa kwenye mechi hizi zijazo za Mapinduzi na ligi kuu.
"Na
hiyo asubuhi yenyewe ni bora tungekuwa tunafanya mazoezi mepesi,
tunafanya mazoezi magumu kwa masaa (saa) mawili kwa jana (juzi) siku ya
mechi asubuhi tulikimbia mbio fupi na ndefu, kuruka koni na kumalizia na
kupiga penalti kitu ambacho siyo sahihi," alisema mtoa taarifa huyo.
Alipotafutwa
Lwandamina bila mafanikio lakini Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma
Mwambusi, alisema: “Katika mechi hii, wachezaji waliingia uwanjani
wakiwa na matumaini makubwa ya ushindi kutokana na mwenendo wa Azam
katika michuano hii.
"Hivyo,
dharau hizo ndizo zikatusababishia tupate matokeo hayo, lakini yote kwa
yote benchi la ufundi limeangalia makosa yaliyojitokeza katika timu na
kusababisha kupata matokeo hayo, hivyo tunajipanga kwa ajili ya mchezo
ujao."
SOURCE: CHAMPIONI
Post a Comment