VIGOGO HAWA NDIYO KIKWAZO CHA CHELSEA KUBEBA UBINGWA ENGLAND, IKIWEZA, BASI MAMBO KWA ULAINIIII
Chelsea iko kileleni mwa Ligi Kuu England kwa tofauti ya pointi dhidi ya Liverpool wanaoshika nafasi ya pili.
Lakini hiyo bado si sababu ya kuamini tayari wao wana nafasi ya kuwa mabingwa na hasa kama utazungumzia mechi za vigogo sita.
Vigogo sita wa Premier League ni Manchester United, Liverpool, Arsenal, Chelsea, Manchester City na Tottenham.
Hakuna ubishi hizi ndiyo timu sita zinazowania ubingwa na lazima bingwa atatoka miongoni mwao.
Kama
utaangalia mechi tano kwa kila timu baada ya kukutana na kigogo mmoja
mara moja, Liverpool ndiyo haikupoteza dhidi ya kigogo yoyote.
Lakini
Chelsea ilipoteza mechi mbili, moja ikichapwa mabao 4-0 na Arsenal. Man
City ilipoteza mechi tatu na zilizobaki zote zilipoteza mechi mbili.
Katika
mechi tano dhidi ya vigogo wenzake, kama utatengeneza msimamo wa vigogo
tu, Liverpool ndiyo inaongoza kwa kukusanya pointi 11 katika mechi hizo
tano ikifuatiwa na Chelsea yenye pointi 9.
Man
Cityi imekusanya 6 huku Arsenal, Spurs na Man United kila mmoja
imekusanya pointi 5 ikiwa ni wastani wa pointi moja kwa kila mechi sawa
na sare 5.
Hii
inaonyesha bado kuna ugumu wa juu kwa Chelsea na analazimika kufanya
vema katika mechi 5 dhidi ya vigogo wenzake ili kujihakikishia ubingwa.
MECHI ZIJAZO ZA VIGOGO SITA:
Jan 4: Tottenham v Chelsea
Jan 15: Man United v Liverpool
Jan 21: Man City v Tottenham
Jan 31: Liverpool v Chelsea
Feb 4: Chelsea v Arsenal
Feb 11: Liverpool v Tottenham
Feb 26: Man City v Man United
Mar 4: Liverpool v Arsenal
Mar 18: Man City v Liverpool
Apr 1: Arsenal v Man City
Apr 5: Chelsea v Man City
Apr 15: Man United v Chelsea
Apr 29: Tottenham v Arsenal
May 6: Arsenal v Man United
May 13: Tottenham v Man United
Post a Comment