Zifuatazo ni baadhi ya sababu kwanini mabinti wengi wanashindwa KUOLEWA HASA MIAKA YA HIVI KARIBUNJ..?👉VIGEZO VISIVYO NA MSINGI.🔹Kuweka vigezo vingi na kuchagua chagua sana wanaume inaweza ikawa ni sababu ya kufanya mabinti wengi wasiolewe. 🔹Binti
unakuta anataka mwanaume awe amesoma, mrefu, handsome boy, anavaa
vizuri awe na hela gari nyumba au awe na kazi nzuri, awe na upendo wa
kweli, na mambo mengi kama hayo. 🔹Wanaume
wanaokidhi vigezo hivyo ni wachache sana na kimsingi inawezekana
wasiwepo kabisa. Mwisho hujikuta umri unaenda bila ya kuolewa au
kuangukia kwenye mikono ya Wanaume ambao ni matapeli wa mapenzi. 🔹kuna msemo usemao, "ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu" na mwingine ufananao na huo unaosema "mchagua nazi hupata koloma". 👉NAMNA UNAVYOJIWEKA. 🔹Jinsi unavyojiweka ndivyo watu watakavyokuchukulia. Mavazi unayovaa, marafiki ulionao na hata tabia yako kwa ujumla. 🔹Mabinti
wengi wanafeli sana kwenye eneo la mavazi, mavazi ya kuacha maungo ya
ndani wazi yanawashushia heshima mabinti wengi sana bila wao kujua,
wengi wanaona kama wanaenda na wakati lakini wanajidhalilisha. 🔹Hakuna
mwanaume anayependa kuoa mwanamke asiyejiheshimu, kama yupo basi
hatakuwa si muaoji. Mwanaume gani anayependa kutembea na mkewe akiwa
maziwa yapo wazi yananing'inia kama yanataka kuanguka? Sketi fupi
mapaja yote yapo wazi na tena ina mpasuo? Suruali imembana mpaka
maumbile ya ndani, michirizi ya nguo ya ndani inaonekana? 🔹Sidhani
kama kuna mwanaume anayependa mwanamke ambaye mwili wake ni maonyesho
ya saba saba, Sidhani kama kuna mwanaume anayependa kuwa na mwanamke
ambaye hata nyumbani kwao hana ujasiri wa kumpeleka. Sidhani kama kuna
mwanaume anayependa kuwa na mwanamke ambaye starehe yake ya usiku na
Mali yake ipo wazi kwa marafiki zake na watu wengine kama Mali ya umma. 🔹Niwasaidie
dada zangu,ukivaa mavazi ya ajabu ajabu utavutia Wanaume wa kulala na
wewe na kukuacha na kukuchezea tu si waoaji, utakuwa ni kiburudisho cha
usiku mmoja na si mwanamke wa maisha. 👉MANENO UNAYOJITAMKIA. 🔹Vijana wengi wamekuwa na desturi ya kujisemea maneno ya laana bila kujua yana madhara gani katika maisha yao. 🔹Utakuta
Binti kwa sababu aliumizwa na kijana fulani basi, anasema Wanaume wote
ni wale wale, sijui siku hizi Hakuna waoaji, mara Wanaume wote ni
waongo, baba mmoja na mama mmoja. 🔹Sikia nikuambie, kinywa chako kina uwezo wa kuumba. Kila neno baya au zuri unalojitamkia ndivyo litakuwa kwako.🔹Kama
Unasema Wanaume wote ni waongo basi usishangae Kila mwanaume
atakayekuja kwako akiwa muongo. Kama Unasema sina shida ya kuolewa basi
miaka 30 itakukuta ukiwa nyumbani kwa baba yako. Chunga kinywa Chako. 👉KUTOKUSHUKA.🔹Utii ni tatizo kwa mabinti wengi sana wa sasa. Wengi hawakubali kushuka, hawataki Kuongozwa wanataka kujiongoza wenyewe. 🔹Kumtii mume wanaona kama ni jambo la kizamani, wanaita mfumo dume hivyo wanataka kuishi katika mfumo Jike. 🔹Napenda kusema wasichana wengi vazi la Suruali limeathiri mpaka fikra zao, hata akili zao pia zimevaa Suruali. 🔹Binti
Hakuna mwanaume anayependa kuwa na mke ambaye si msikivu (jike dume),
kama hautaki Kuongozwa basi wewe ni mwanaume sasa unataka mwanaume wa
nini? 🔹Mwenyezi mungu anasema hakika mwanaume ni kiongozi mbele ya mwanamke. 🔹Binti kaa kwenye nafasi yako. Jivike kiremba cha Hekima na Utii. 👉MAAGANO ULIYOWEKA HUKO NYUMA.🔹Kama
kuna mtu mliahidiana kuwa mtaona halafu kwa sababu zisizo na msingi
ukamuacha, basi hii inaweza ikawa ni moja ya sababu ya kukufungia baraka
yako na rizki ya ndoa. 🔹Kama
kuna mtu ana nung'unika kwa ajili yako, kama kuna mtu ana lia kwa ajili
yako huu unaweza ukawa mwiba kwako usiifikie ndoa au ukaifikia lakini
isiwe salama. 🔹Kama
kuna watu ulishindwa kutimiza ahadi uliyowaahidi unatakiwa kutubu
dhambi hiyo na kutengeneza nao kwa kuwaomba msamaha ili usiwe na vifungo
vinavyokuzuia.👉KUKOSA MSIMAMO.🔹Mabinti wengi sasa hawana msimamo linapokuja swala la kujizuia kufanya mapenzi.🔹Nimewafanyia counselling mabinti wengi na zaidi ya 80% kama si 90% wanalalamika kuumizwa na wapenzi wao. Ninapowauliza kama walishafanya sex karibu wote wanajibu NDIO.🔹Kama mwanaume umeshampa mwili wako ni nini tena atakachokihitaji kutoka kwako? Kama ameshakula sebuleni kuna haja gani ya kuingia Jikoni? Hahahaa.🔹Ukivua Sketi yako kabla ya ndoa, usitegemee kuvaa gauni (shela) la ndoa. Duh? Hatariiii.👉ROHO CHAFU.🔹Zipo
roho chafu (mapepo) zinazoweza kumfunga mtu asioe au kuolewa. Kuna
wengine wamefunga ndoa za kipepo na majini mahaba na kuota wanafanya
mapenzi na wanaume wasiowafahamu.🔹Pia
zipo roho zinazofuatilia ukoo toka kizazi hadi kizazi wasiingie kwenye
ndoa. Unakuta watoto wa familia fulani wote hawajaoa au kuolewa. KEMEA ROHO MCHAFU HUYO Badilikeni wanawakeeeeee!
Post a Comment