Rais Magufuli amvua ubunge na Uwaziri Dkt. Possi......Amteua Kuwa Balozi

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo
tarehe 19 Januari, 2017 amemteua Dkt. Abdallah Possi kuwa Balozi.
Kituo cha kazi na tarehe ya kuapishwa kwa Dkt. Abdallah Possi itatangazwa baadaye.
Kabla
ya uteuzi huo Dkt. Abdallah Possi alikuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu aliyekuwa
akishughulikia Ulemavu.
Kufuatia
uteuzi wa Dkt. Abdallah Possi kuwa Balozi, nafasi ya Naibu Waziri,
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu
(Ulemavu) itajazwa baadaye.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
19 Januari, 2017
Post a Comment