Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco Atumbuliwa
Rais John Pombe Magufuli, ametengua
uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania
(Tanesco), Mhandisi Felschemi Mramba kuanzia leo, Januari 1, 2017.
Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Ikulu, Gerson Msigwa, Rais Magufuli amemteua Dkt.
Tito Esau Mwinuka kuwa kaimu mkurugenzi wa shirika hilo. Kabla ya uteuzi
huo, Mwinuka alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM).
Post a Comment