Mbowe atembelea shamba lake lililopigwa marufuku na Serikali
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjbZhIvLO1zBN07IrYODESgZneJYrGooCYp8AdNy63KGzzbz5Jb6a9tc0-Y0gYHDGP7p1mY7ClqZrJcCdCBGzoPgUNQ0qkAWsyTJauaYB_ihiVh5adQT5xZTAdFblorJEX9XcDo-TfHV2I/s1600/1.jpg)
Mwenyekiti
wa Chadema ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe ametembelea
shamba lake la kilimo cha kisasa cha mboga mboga ( Green House) yaliyopo
Hain na kuwajulia hali wafanyakazi pamoja na wataalam wake leo Ijumaa.
Pia,
Mbowe amepata wasaa ya kuzungumza na baadhi ya wafanyakazi ambao
walimweleza hofu kubwa waliyoingiwa nayo ya kupoteza ajira zao
wanazozitegemea katika kuendesha maisha yao ya kila siku.
Hali
hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasiu Byakanwa kupiga
marufuku shughuli za kilimo zinazoendeshwa na shamba la Kilimanjaro
Veggies linalomilikiwa na Mbowe.
Byakanwa
alitoa amri hiyo baada ya kutembea shamba hilo lenye ukubwa wa hekari
mbili akisema kilimo hicho ni kinyume cha sheria kwani shamba hilo lipo
ndani ya mita 60 kutoka mto Weruweru.
Post a Comment