LUNYAMILA AMZUNGUMZIA NGOMA, ASEMA ANGEKUWEPO ANGEMALIZA MCHEZO

Winga
hatari wa Yanga, Edibily Lunyamila amesema kikosi cha Yanga dhidi ya
Simba, kilimkosa Donald Ngoma kama pacha wa Amissi Tambwe.
Watani
hao walivaana katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi kwenye
Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar, jana. Simba ilishinda mikwaju 4-2 ya
penalti.
Lunyamila anaamini iwapo Ngoma raia wa Zimbabwe angecheza katika mechi hiyo, basi mechi hiyo ingeisha ndani ya dakika 90.
"Ngoma angesaidia kuamua matokeo ya mechi. Beki ya Simba haikuwa makini sana, haikuwa na mtu wa kuwasumbua sana," alisema.
Ngoma anajulikana kwa usumbufu wa hali ya juu usiowapumzisha mabeki wa timu pinzani lakini ana uwezo wa kufunga pia.
Ngoma ni majeruhi na katika mechi hiyo nafasi yake ilichukuliwa na Deus Kaseke huku Tambwe akicheza namba kumi.
Hata hivyo, Tambwe alishindwa kuonyesha cheche kutokana na Simba kujaza viungo wengi na kukaba zaidi.
Hata hivyo, Yanga ndiyo ilipoteza nafasi nyingi zaidi za kufunga katika mechi hiyo.
Post a Comment