Jeshi la Polisi Laua Majambazi Watatu Dar es Salaam
Watu
watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, wameuawa katika tukio la
kurushiana risasi na polisi katika eneo la Mikocheni, karibu na Shule ya
Sekondari Feza jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon
Sirro watuhumiwa hao waliuawa jana asubuhi na majina yao bado
hayajafahamika.
Alisema
marehemu hao ni waliohusika katika tukio la kupora zaidi ya Sh milioni
26 katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere, eneo la Tazara,
Dar es Salaam.
Hata
hivyo, alipoulizwa ufafanuzi zaidi wa tukio hilo na je watuhumiwa hao
walikuwa na usafiri gani, Sirro alisema kuwa hizo ni taarifa za awali na
taarifa rasmi atazitoa leo.
Alisema kwamba miili ya marehemu, imehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Taarifa
zaidi zinadai kwamba watuhumiwa hao akiwemo mwanamke aliyejisalimisha,
ambaye ndiye alikuwa dereva wao, walikuwa na mpango wa kufanya uvamizi
katika maeneo hayo, ambapo pia baadhi yao walifanikiwa kukimbia.
Lakini, Polisi haijathibitisha taarifa hizo na imeeleza kuwa itatoa taarifa zaidi leo.
Post a Comment