ad

ad

January Makamba Alivyoadhimisha Kuzaliwa Kwake Bumbuli







 Januari 28 kila mwaka ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, na Mbunge wa Bumbuli, January Yusuf Makamba.

Katika siku yake ya kuzaliwa mwaka 2017, Waziri Makamba aliiadhimisha tofauti ambapo alikwenda jimboni kwake na kushiriki shughuli mbalimbali na wapiga kura wake.

Makamba alipata nafasi ya kushiriki shughuli za ujenzi jimboni Bumbuli lakini pia alifanya vikao na watu mbalimbali vyenye lengo la kujadili mustakabali wa maendeleo ya jimbo hilo.

Mbali na hayo Makamba alitembelea baadhi ya shule za msingi jimboni humo na kuzungumza na wanafunzi huku akiwahimiza kuweka bidii kwenye masomo yao kwani Bumbuli na Tanzania inawategemea wao kuja kuwa wataalamu wa baadaye wa kuisaidia.

Makamba anatimiza umri wa miaka 43 tangu azaliwe 28 Januari 1974 mkoani Singida.


No comments

Powered by Blogger.