Ronaldo Anyakuwa Ballon d’Or, Awavurugua Messi, Griezmann na Suarez
Unaweza kusema huu ni mwaka wa Cristiano Ronaldo hata kama unakwenda ukingoni.
Maana amefanikiwa kushinda tuzo ya
mwanasoka bora wa dunia maarufu kama Ballon d'Or . Ronaldo sasa
anaichukua mara ya nne, akiwa alianza mwaka 2008 akiwa Manchester United
na alipoingia Madrid, unaweza kusema hii ni 'hat trick'.
Kabla haijawa Ballon d'Or, Ronaldo alichukua mwaka 2008, Messi akachukua mwaka 2009.
Baada ya kuwa Ballon d'Or, Messi amechukua mara nne miaka ya 2011, 2012, 2013 na 2015. Huku Ronaldo akiwa amechukua mara tatu katika miaka ya 2013, 2014 na 2016.

Kumbuka alishinda Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Real Madrid, akashinda Kombe la Euro akiwa na Ureno.
Leo amebeba kura zaidi kati ya 173
zilizopigwa na waandishi duniani kote kwa usimamiza wa jarida maarufu la
Ufaransa la France Football na kuwapiga bao Antoine Griezmann wa
Atletico Madrid na Luis Suarez na Lionel Messi, wote wa Barcelona.

Post a Comment