Manchester City Yasherekea Ushirikiano Wa Kimataifa Na Tecno Mobile
Watengezaji
wakubwa wa simu za mkononi TECNO Mobile na Klabu ya ligi ya Uingereza,
Manchester City leo wanasherehea uzinduzi wa ushirikiano wa kimataifa
kwa miaka kadha.
Kama mshirika rasmi wa Klabu ya mpira ya Manchester City, TECNO Mobile itashirikiana na klabu hiyo kukuza mikakati ya masoko na matangazo ya kampeni sehemu mbalimbali duniani, ikiwemo bara la Afrika ambapo TECNO tayari inatambulika kama kinara wa soko la simu za mkononi.
TECNO
ambayo ni sehemu ya Transsion Holdings, kwa mara ya kwanza ilianzishwa
nchini China na kwa miaka kumi iliyopita imekuza umaarufu wake katika
masoko tofauti zaidi ya 40 yanayochipukia ambako mashabiki wa Manchester
City wapo na wanaendelea kuongezeka kila siku.
Akizungumza
kwenye uzinduzi wa ushirikiano huo wa kimataifa uliofanyika kwenye
kituo cha mafunzo na uangalizi wa maendeleo ya vijana, Afisa Mkuu wa
Biashara wa City Football Group Tom Glick alisema “Tunafurahi
kuwakaribisha TECNO Mobile katika mkusanyiko wa ushirikiano wa
kimataifa, kujikita kwake zaidi katika masoko ya nyumbani kunaendana na
namna ambavyo tunafanya shughuli zetu na tunatazamia kushirikiana nao
kuungana na mashabiki wa Manchester City duniani kote.
Stephen
Ha Mkurugenzi Mtendaji wa TECNO Mobile akizungumza katika uzinduzi
katika kituo cha mafunzo na uangalizi wa maendeleo ya vijana cha
Manchester City aliongezea:
“Tunashukuru
sana kushirikiana na klabu yenye mafanikio na inayojulikana ya
Manchester City, tutaendeleza uhusiano wetu wa muda mrefu katika michezo
kwa hali ya juu”
“Kwa
kuwapatia wateja wetu uzoefu wa kufurahia zaidi simu bora
isiyolinganishwa na nyingine ni kipaumbele cha juu kwa TECNO Mobile na
tunaona ulinganifu mwingi mno na Manchester City tukiangalia mkazo wao
wanaoweka katika kuwapatia mashabiki wake uwezo wa kufurahia utofauti wa
kipekee kwa njia ya mtandao.
“Tunafuraha kujiunga na timu yao na tunasubiri kwa hamu kuanzisha ushirika huu pamoja."
Post a Comment