Kikosi Cha Azam Kuhamia Kujiweka Sawa
Kikoai
cha Azam FC, keshokutwa Jumatano kinatarajiwa kwenda visiwani Zanzibar
kuweka kambi ya muda mfupi ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu
Bara unaotarajiwa kuanza Desemba 17, mwaka huu.
Timu
hiyo ambayo imemaliza mzunguko wa kwanza ikiwa nafasi ya tatu na pointi
25, imedhamiria kufanya kweli mzunguko wa pili huku ikifanya usajili wa
maana kwa kuwanyakua Waghana watatu, Enock Atta Agyei, Yahaya Mohammed
na Samuel Afful.
Meneja
wa timu hiyo, Philip Alando, amesema leo Jumatatu kikosi chao rasmi
kitaanza mazoezi huku keshokutwa Jumatano wakitarajiwa kwenda visiwani
humo.
“Ni
kweli tunaenda Zanzibar kama hakutakuwa na mabadiliko yoyote kwani
kocha mkuu, Zeben Hernandez ndiye aliyepanga kambi iwe huko, hivyo kama
akiendelea kushikilia msimamo wake huo, basi Jumatano tutapanda boti na
tutakaa kwa siku tano mpaka kumi,” alisema Alando.
Post a Comment