Jide Akiri Kutoka Kimapenzi na Mnigeria Spicy ‘Rasta’
HATIMAYE staa wa muda wote
katika muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ a.k.a Jide jana amekiri bila kupepesa maneno kuwa yupo katika penzi zito na
mwanamuziki mwenzake raia wa Nigeria aitwaye Chris maarufu kama Spicy a.k.a Rasta.
Jide ameyafunguka hayo wakati akifanya
Exclusive Interview na Global TV Online kwenye studio zake zilizopo
ndani ya Ofisi za Global Publishers Ltd eneo la Bamaga, Mwenge jijini
Dar es Salaam.
Mbali na kuwa katika mahaba na Rasta,
Jide amefunguka kuwa tayari wana project ambayo anaifanya na mpenzi wake
huyo na inatarajiwa kuwa mtaani kesho Jumatano ya Desemba 14, 2016.
Global TV Online ilimtupia swali mpenzi
wa Jide ikimuuliza kuwa ni wapi alikutana na mrembo huyo, na haya ndiyo
yalikuwa majibu ya Rasta.
“Aaah, i can’t explain it here, but i
didn’t meet Jide in Tanzania” akimaanisha kuwa hawezi kuelezea kuhusu
mahusiano yake na Jide lakini hakukutana naye hapa Tanzania.
Jide kwa upande wake anasema alikutana
na Rasta katika kazi zao za muziki maana wote ni wasanii kama ambavyo
wafanyakazi wa benki wanaweza kuingia katika mapenzi kwa kuwa wote wapo
karibu kikazi.
Spicy alipoulizwa ni mpango gani anao na dada yetu alisema wanapendana na mambo mengine yatajulikana kadri muda unavyokwenda.
Kuhusu tuzo aliyoipata juzi katika EATV
Awards 2016 ya Mwanamuziki Bora wa Kike, Jide alisema amejisikia vizuri
na imemtia nguvu katika kazi yake ya muziki.
Global TV Online ilimtupia swali lingine
Jide kuhusu mbinu gani aliyotumia kumchunguza mpenzi wake huyo, ambapo
alisema hakutumia muda mwingi kumjua na kwamba walipokutana walijikuta
wamezama katika mapenzi hivyo haikumchukua muda mrefu kufikiria hilo.

Post a Comment