DARASSA ASIMULIA AJALI ILIVYOKUWA, AELEZA CHANZO HADI ILIPOTOKEA
Msanii
wa hip hop anayetamba hivi sasa na wimbo wake wa Muziki, Sharrif
Thabeet ‘Darassa’ amesema kuwa hataki kuamini imani za kishirikina
kuhusika kwenye ajali aliyoipata huku akitamka yote hayo ni mipango ya
Mungu.
Kauli
hiyo, ameitoa ikiwa ni siku moja tangu anusurike kifo akiwa na ‘crew’
yake baada ya kupata ajali maeneo ya Ntobo barabara ya kuelekea Mgodi wa
Bulyanhulu Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, akiwa anaelekea kwenye
shoo.
Darassa
alipata ajali hiyo ya gari akiwa na maprodyuza wake Remmy Raymond ‘Mr
VS’, Habbar na dairekta wake Hanscana wakiwa kwenye gari aina Toyota
Harrier.
Darassa
amesema gari lao halikuwa spidi kiasi cha kusababisha wao wapate ajali,
lakini ghafla aliona usikani ikikataa kurudi kutoka kulia kuja kushoto
eneo walilokuwa wanaelekea.
“Kiukweli
kabisa nikwambie tu, hakukuwa na tatizo lolote katika safari yetu,
nilishangaa ghafla kuona gari lenyewe likielekea upande wa kulia na
kikubwa cha kushukuru hatukuwa kwenye mwendo wa kasi.
“Ninaamini
kama ningekuwa naendesha kwa mwendo wa kasi, basi sidhani kama
tungetoka kwenye ajali hii tuliyoipata na kitu kingine cha kushangaza
hakukuwa na chanzo chochote cha ajali kwa maana labda mbele au nyuma
yetu kulikuwa na gari lingine, tulikuwa wenyewe.
“Mimi sitaki kuamini kama nimerogwa bali namshukuru Mungu tu,”alisema Darassa.
SOURCE: CHAMPIONI


Post a Comment