Waziri mkuu nchini DRC ajiuzulu
Wadhifa wa bwana Ponyo utachukuliwa na mwanachama wa upinzani
Waziri mkuu nchini Jamhuri ya
Demokrasi ya Congo Augustin Matata Ponyo, amejiuzulu na kutoa fursa ya
kuteuliwa mrithi wake kuongoza serikali ya mpito.
Wapiga kura nchini DRC walistahii kupiga kura mwezi huu kumchagua mrithi wa Rais Kabila, wakati wa kumalizika kwa muhula wake wa mwisho.
Vyama vikuu vya upinzani vinakataa kuhairishwa kwa uchaguzi vikisema kuwa hiyo ni njama ya Rais Kabila ya kusalia madarakani.
Baraza lote la mawaziri lilijiuzulu pamoja na bwana Ponyo.
CREDIT: BBC SWAHILI

Post a Comment