Samir Nasri: Guardiola huwataka wachezaji kutofanya mapenzi baada ya saa 6 usiku
Mchezaji wa Ufaransa katika safu ya
kati Samir Nasri amefichua kwamba mojawapo ya ufanisi mkubwa wa mkufunzi
Pep Guradiola ni kuwaagiza wachezaji wake kutofanya mapenzi baada ya
saa sita usiku.
Katika mahojiano na runinga ya Ufaransa,Nasri
amesema kuwa Guardiola aliweka sheria hiyo hata iwapo kungekuwa hakuna
mechi siku iliofuatia ili wachezaji wapate usingizi mwanana.Hata Lionel Messi anayetambulika kuwa mchezaji bora duniani hakuwachwa nje wakati wa uongozi wa Guradiola katika timu ya Barcelona.
Nasri amesema kuwa hatua hiyo ilimwezesha Messi kutopata majeraha ya misuli

Post a Comment