JPM Aikosa Tuzo ya Person of the Year 2016 Inayotolewa na Forbes
Madonsela.
Aliyekuwa Mwendesha Mashtaka wa
Serikali na Wakili nchini Afrika Kusini Thuli Madonsela jana ametangazwa
kuwa ndiye mshindi wa Tuzo ya Mtu Mashuhuri Afrika ya Forbes (Person
of the Year #POY2016).
Tuzo huyo hupewa mtu aliyetoa mchango
mkubwa katika kuiinua jamii kwenye njanja mbalimbali za maisha kama vile
uchumi, siasa, utamaduni.
Katika kinyang’anyiro cha tuzo hiyo,
Thuli Madonsela alikuwa akichuana na Michiel Le Roux kutoka Afrika
Kusini, Rais wa Mauritania, Ameenah Gurib, Jamii ya watu wa Rwanda na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.
Mwaka 2015 tuzo hii ilikwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya MeTL, Mohammed Dewji.


Post a Comment