MECHI ZA LIGI KUU TANZANIA BARA LEO, AZAM, YANGA, SIMBA WAKO UWANJANI....
| AZAM FC |
Leo Oktoba 19, mwaka huu kuendelea kwa mechi sita pia za mzunguko
11 wa kukamilisha raundi ya kwanza kwa msimu 2016/17.
Vodacom
– Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza nchini kwa kutoa huduma za
kisasa za mawasiliano ndiyo mdhamini mkuu ligi hiyo ikisaidiana kwa
karibu sana Kampuni ya kisasa ya vyombo vya habari yenye kurusha vipindi
vyake kwa weledi na ubora wa hali ya juu ya Azam Televisheni (Azam Tv)
na DTB- Benki ya kuaminika nchini kwa usalama wa fedha zako.
Kampuni
hizo zinazong’arisha VPL, kesho zitakuwa sambamba kwenye kuchagiza
michezo ya Ruvu Shooting ya Pwani ambayo itaikaribisha Mwadui ya
Shinyanga kwenye Uwanja wa Mabatini uliuoko Mlandizi mkoani Pwani katika
mchezo Na. 81 wa VPL utakaoanza saa 10.00 jioni.
Mchezo
Na. 82 utakaozikutanisha Azam FC ya Dar es Salaam na Mtibwa Sugar ya
Morogoro utafanyika saa 1.00 usiku (19h00). Mchezo huo utafanyika Uwanja
wa Azam ulioko Chamazi – maskani ya Azam yalioko nje kidogo ya jiji la
Dar es Salaam wakati mchezo Na. 83 utazikutanisha timu za Ndanda FC na
Mbeya City ya Mbeya kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Mchezo
Na. 85 utazikutanisha timu za Tanzania Prisons ya Mbeya na Stand United
itakayokuwa mgeni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya
huku mechi Na. 87 itazikutanisha Toto African ya Mwanza itakayocheza na
Young Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati African
Lyon itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Uhuru,
jijini Dar es Salaam kwenye mchezo Na. 88.
Ligi
hiyo itaendelea tena keshokutwa Alhamisi Oktoba 20, kwenye Uwanja wa
Uhuru, Dar es Salaam ambako vinara wa ligi hiyo kwenye msimamo hadi
sasa, Simba itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza katika mchezo Na. 84.
Post a Comment