Makamuzi Ya Twanga Ndani Ya Toroka Uje
Bendi ya
African Stars ‘Twanga Pepeta’ Kisima cha Burudani, usiku wa kuamkia leo
imefanya makamuzi ya nguvu kwenye Ukumbi wa Toroka Uje, uliopo Tabata Jijini
Dar, ikiwa ni maazimisho ya kumbukumbu ya Hayati Baba wa Taifa, Hayati Julius
Nyerere ‘Nyerere Day’.
Kama kawaida
kundi zima la bendi hiyo likiongozwa na Ally Choki ‘Mzee wa Farasi’
liliwanogesha mashabiki na kuwafanya kuvamia steji na kujiachia kimadaha.
Bendi hiyo
imeufanya ukumbi huo kuwa ukumbi wake wa nyumbani ambapo ‘itakongoli’ kila
Ijumaa.
Post a Comment