Wastara Apata Ubalozi wa Simu za KZG, Atalipwa shilingi Milioni Mia Nne Kwa Mwaka
Wastara
(katikati) akisaini mkataba huo.
Meza kuu wakionyesha aina za simu hizo.
Staa wa
filamu Bongo, Wastara Juma amepata shavu la kuwa balozi wa Kampuni ya simu ya
mkononi ya KZG ambapo leo amekabidhiwa na kusainishwa mkataba rasmi.
Akizungumza
katika tukio la kusaini makubaliano ya kuwa balozi wa kampuni hiyo lililofanyika katika ukumbi wa De Mag Hotel
iliyopo Mwananyamala, Dar, Wastara
alisema amefurahi sana kupata shavu hilo kwani kujituma kwake katika biashara
ndiko kulikompatia bahati hiyo.
Aliendelea
kusema kwamba atahakikisha anafanya vizuri katika ubalozi huo ambao kwa mwaka
unampatia shilingi milioni mia nne kutegemea na jinsi kampuni hiyo inavyouza
bidhaa zake hizo kwani imempa heshima kubwa ambayo hakuitarajia.
“Nina furaha
sana kuwa balozi wa KZG, hii imetokana na kujituma kwangu kwani ninafanya
biashara nami ni mwanamke ambaye ninajitambua na najua ninachokifanya,
naishukuru kampuni hii kwa kuniona hivyo, naomba mashabiki zangu waniunge mkono,”
alisema Wastara.
Katika tukio
hilo pia kampuni hiyo ilimzawadia keki Wastara ikiwa ni zawadi ya kumbukumbu ya
kuzaliwa kwake kwani ilikuwa jana, hivyo kutokana na nafasi hiyo wakaona ni
vyema wampe zawadi hiyo iliyokuwa imechorwa aina mojawapo ya simu za KZG.
Post a Comment