Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa akinadi vitu mbalimbali
katika harambee hiyo kuchangisha fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa
huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta,
harambee iliyoendeshwa na Kanisa la Deliverance Centre Victorius (CVC),
chini ya Mchungaji Jehu Mkono.
Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa akizungumza katika harambee
hiyo kuchangisha fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto
wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta, harambee iliyoendeshwa
na Kanisa la Deliverance Centre Victorius (CVC), chini ya Mchungaji
Jehu Mkono.
MBUNGE
wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa ameongoza harambee ya uchangishaji
wa fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika
mazingira magumu eneo la Tegeta, harambee iliyoendeshwa na Kanisa la
Deliverance Centre Victorius (CVC), chini ya Mchungaji Jehu Mkono.
Harambee hiyo ilifanyika katika Kanisa la Deliverance Centre Victorius
Tegeta kwa Ndevu, jijini Dar es Salaam, ambapo Bonnah Kaluwa alikuwa
mgeni rasmi na kufanikiwa kukusanya fedha shilingi 13,730,000 ambazo
zilipatikana kwa michango ya waumini, wageni waalikwa na kufanyika kwa
mnada ulionadi vitu anuai.
Katika
harambee hizo Mbunge, Kaluwa alitoa shilingi milioni mbili yeye pamoja
na mumewe huku akiendesha mnada uliotunisha mfuko wa ujenzi wa kituo
hicho. Awali akizungumza katika harambee hiyo Mwenyekiti wa umoja wa
akinamama wa kanisa la CVC, Rose Haji Mwalimu alisema harambee hiyo
itawezesha kupatikana kwa fedha za ujenzi wa kituo pamoja na upanuzi wa
kanisa la CVC eneo la Tegeta mradi unaotarajia kutumia shilingi milioni
40.
Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa (wa tatu kulia) akikata keki
kuashiria uzinduzi wa harambee hiyo iliyoendeshwa na Kanisa la
Deliverance Centre Victorius.
Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa (wa pili kulia) akipeana
mkono na Mwenyekiti wa umoja wa akinamama katika Kanisa la Deliverance
Centre Victorius, Rose Haji Mwalimu (kulia) mara baada kukabidhi risala
ya ujenzi wa kituo hicho. Kushoto ni Hoyce Temu, ambaye ni mwanakamati
wa harambee hiyo.
Meza kuu ikimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa (hayupo
pichani akizungumza) katika harambee ya uchangishaji wa fedha za ujenzi
wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu
eneo la Tegeta, harambee iliyoendeshwa na Kanisa la Deliverance Centre
Victorius (CVC).
Askofu Fedrick Ndonde (kushoto) ambaye ni rafiki wa karibu wa Kiongozi
Mkuu wa CVC Deliverance Centre Victorius, Mchungaji Jehu Mkono
akizungumza katika hafla hiyo.
Hoyce Temu (kushoto) ambaye ni mwanakamati wa harambee ya uchangishaji
wa fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto wanaoishi katika
mazingira magumu eneo la Tegeta, harambee iliyoendeshwa na Kanisa la
Deliverance Centre Victorius (CVC) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Segerea,
Bonnah Kaluwa na mgeni rasmi katika hafla hiyo.
Kiongozi Mkuu wa CVC Deliverance Centre Victorius, Mchungaji Jehu Mkono
(kulia) akishusha maombi kabla ya kuanza kwa harambee hiyo ya
uchangishaji wa fedha za ujenzi wa kituo cha kutoa huduma kwa watoto
wanaoishi katika mazingira magumu eneo la Tegeta.
Baadhi ya wageni waalikwa katika harambee iliyoendeshwa na Kanisa la
Deliverance Centre Victorius (CVC), chini ya Mchungaji Jehu Mkono wakiwa
katika harambee hiyo.
Mwimbaji wa muziki wa injili, Edson Mwasabwite (kulia) akitumbuiza
katika hafla hiyo ya uchangishaji fedha huku akiungwa mkono na Mbunge,
Bonnah Kaluwa na viongozi wengine.
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Deliverance Centre Victorius Tegeta kwa
Ndevu, jijini Dar es Salaam, wakiwa katika harambee hiyo.
Kutoka kushoto ni Askofu Fedrick Ndonde, mwanakamati wa harambee hiyo,
Hoyce Temu pamoja na Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa wakiwa
katika harambee hiyo.
Kiongozi Mkuu wa CVC Deliverance Centre Victorius, Mchungaji Jehu Mkono
(katikati) akiahidi kuchangia shilingi milioni moja katika mradi huo.
Post a Comment