Rasmi Simba imeingia mikataba na mastaa watano wa kimataifa akiwemo Mavugo
Klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba ambayo mwaka huu inajiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu soka Tanzania bara sambamba na sherehe za miaka 80 ya klabu hiyo, ambayo itaadhimishwa siku ya Simba Day August 8 2016, leo August 5 2016 imetangaza kuingia mikataba na mastaa watano wa kimataifa.
Laudit Mavugo akisaini mkataba na Rais wa Simba Evans Aveva kushoto
Simba ambao wameingia mikataba na mastaa hao akiwemo mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi waliyemuwinda kwa zaidi ya misimu miwili Laudit Mavugo, wamefanikiwa kuwasajili pia Fredric Blagnon kutokea Ivory Coast, Musa Ndusha, Janvier Bokungu na Method Mwanjale.
Janvier Bokungu na Rais wa Simba Evans Aveva
Mastaa wote wa kimataifa waliosajiliwa na Simba watatambulishwa rasmi siku ya Simba Day August 8 2016 uwanja wa Taifa Dar es Salaam, huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Janvier Bokungu
Fredric Blagnon
Fredric Blagnon
Method Mwanjale
Musa Ndusha
Musa Ndusha na Rais wa Simba Evans Aveva
Post a Comment