MO DEWJI AANZA FUJO SIMBA, AMWAGA MILIONI 100 ZA USAJILI
Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Makampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji akimkabidhi Rais wa Simba, Evans Aveva mfano wa hundi ya Sh. Milioni 100 leo mjini Dar es Salaam
MFANYA biashara maarufu hapa nchini, Mohamed
Dewji ‘Mo’, leo hii ameikabidhi klabu ya Simba kitata cha shilingi milioni 100
kama mchango wake kwa ajili ya kuisaidia klabu hiyo katika zoezi zima la
usajili.
Simba ilikuwa
inakabiliwa na uhaba wa fedha ili iweze kukamilisha usajili wake kwa ajili ya
msimu ujao wa Ligi Kuu Bara unaotarajia kuanza kutimua vumbi, Agosti 20 mwaka
huu.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa fedha hizo
Rais wa Simba, Evans Aveva amesema kuwa kiasi hicho kitasaidia kupunguza mzigo
mkubwa walio kuwa wameubeba ili kukamilisha zoezi hilo la usajili.
“Mpaka kufikia sasa tulikuwa tunadaiwa
shilingi milioni 420 ili kukamilisha usajili wetu, lakini kwa kiasi hiki cha
fedha ambazo Mo ametupatia kimetusogeza na tumebakiza milioni 320 ili kukamilisha
zoezi hilo.
“Tunawaomba wanachama wetu wengine ambao wataguswa
na hali hiyo waweze kutusaidia kama alivyofanya Mo.”
Post a Comment