HANS POPPE AHOJI...KAMA FEDHA ZA SAMATTA ZILIPITIA KWENYE AKAUNTI YA MKE WA RAGE, TATIZO NINI ZA OKWI KUWEKWA KWENYE AKAUNTI YA AVEVA?
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema haoni kama
kuna tatizo kwa uongozi wa Simba kuamua kuweka fedha zake kwenye akaunti
ya mwenyekiti wake huku akisisitiza hata fedha za mauzo ya Mbwana
Samatta, zilipitia kwenye akaunti ya aliyekuwa mwekiti wao wa zamani.
Hans
Poppe amesema, kama kweli Aveva alishikilia na kulazwa rumande eti kwa
kuwa fedha za malipo ya Emmanuel Okwi dola 300,000 kutoka Etoile Du
Sahel, basi anashangazwa sana.
“Kweli hilo ni suala la mtu kushikiliwa hadi kulazwa ndani? Kama kweli suala ni hilo, basi ninaamini kutakuwa na tatizo jingine.
“Fedha
za Simba kupitia kwenye akaunti ya kiongozi wala si tatizo, mbona fedha
za Samatta kutoka TP Mazembe zilipita kwenye akaunti ya (Ismail) Rage,
sasa mbona hakukuwa na tatizo?” alisema Hans Poppe.
Aveva
alishikwa juzi na kulala katika kituo cha polisi cha Urafiki jijini Dar
es Salaam, lakini kumekuwa na mkanganyiko kwa kuwa Takukuru, hawajasema
lolote kuhusiana na kushikiliwa kwake ingawa taarifa zimezagaa kuwa ni
fedha za malipo ya Okwi kuhamishwa kutoka kwenye akaunti ya Simba na
kuwekwa kwenye akaunti yake.
Inaelezwa,
kwa pamoja walikubaliana kuziweka kwenye akaunti ya Aveva. Tayari,
baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji pia wameitwa kuhojiwa ingawa
haijajulikana ni akina nani.
Post a Comment