DAKIKA 4, SAMATTA AFANYA 'MAUAJI' UBELGIJI KRC GENK IKIITWANGA LOKEREN BAO 3-0
Mbwana
Samatta ameendelea kuonyesha kwamba uwezo anao baada ya kufunga mabao
mawili wakati kikosi chake cha Genk kikiitwanga Lokeren katika Ligi Kuu
ya Ubelgiji kwa mabao 3-0.
Leon
Bailey ndiye alifunga bao la tatu lakini Samatta alitumia dakika nne
kufunga mabao yake mawili akianza na lile la dakika ya 34 kabla ya
kufunga tena dakika ya 38.
Ushindi
huo unaifanya Genk izidi kuwa imara huku Samatta aliyejiunga na timu
hiyo akitokea TP Mazembe ya DR Congo akizidi kujenja imani kwamba
anaweza na anastahili kuwa anaanza kama ilivyokuwa jana.
Post a Comment