Wateja wa Vodacom Kujichagulia Vifurushi Wavitakavyo #YaKwako2
Katika dhamira yake ya kufanya ubunifu wa teknolojia kwa ajili ya
kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia kwa
kuwapatia huduma bora za kurahisisha maisha na kwa gharama nafuu leo
kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imezindua ofa mpya maalum kwa
wateja wake inayojulikana kama “Ya kwako tu” itakayowawezesha kujipatia
vifurushi vya gharama nafuu kwa kadri ya matakwa yao wapendayo kuanzia
vya huduma ya kuperuzi intaneti (Mitandao ya kijamii, Youtube, Whatsapp
na kadhalika),kupiga simu (Kuenda mitandao yote) na kutuma ujumbe mfupi
wa maneno.
Ili kupata huduma ya ofa hii ya“Ya kwako tu” mteja anachotakiwa kufanya ni kupiga simu namba*149* 03# kupata orodha ya huduma anayohitaji kutumia.

Ili kupata huduma ya ofa hii ya“Ya kwako tu” mteja anachotakiwa kufanya ni kupiga simu namba*149* 03# kupata orodha ya huduma anayohitaji kutumia.
Mkurugenzi wa mawasiliano na Uhusiano
wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (katikati) akifafanua jambo wakati
wa Uzinduzi ya huduma mpya ya ”Ya kwako tu” itakayowawezesha wateja wa
kampuni hiyo kujipatia vifurushi vya gharama nafuu kadri ya matakwa yao
wapendayo kuanzia vya huduma ya data,kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi
wa maneno. Ili mteja aweze kujiunga na huduma hii anatakiwa kupiga
namba*149* 03# na kuchagua ofa ya kwako tu, anayeshuhudia kushoto ni
Afisa Mkuu wa Idara ya masoko wa kampuni hiyo, Ashutosh Tiwary na Mkuu
wa kitengo cha wateja wakubwa wa kampuni hiyo, Danilo De Sousa.
Waandishi wa habari wakiwa kazini.

Post a Comment