Rais Magufuli kwenye baraza la Eid El Fitri leo Dar es salaam
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo July 06
2016 amehutubia Baraza la Eid el-Fitr kwa mara ya kwanza tangu
achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lililofanyika
kitaifa katika viwanja vya Karimejee Jijini Dar es salaam.
Katika hotuba yake amemupongeza Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ali kwa juhudi zake za kuwaunganisha waislamu wote na kupanua uwigo wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kutoa huduma za kijamii na ameahidi kuwa serikali ya awamu ya tano itaunga mkono juhudi hizo.
Rais Magufuli na Sheikhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum mara baada ya kuwasili.
Rais
Magufuli na Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi mara baada ya
kuwasili katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya Baraza la Eid Elfitri.
.
Aidha Rais Magufuli amezungumzia juhudi zinazofanywa na BAKWATA katika kuimarisha taasisi zake zinazotoa huduma za kijamii na kulinda mali zake akisema serikali itahakikisha mali zote za waislamu zinakuwa salama na kwamba wote waliodhulumu mali za waislamu watazirejesha.
.
.
.
Rais Magufuli na Mufti Mkuu Sheikh Aboubakar Zubeir.
.
.

Post a Comment