Ndondo Cup 2016: Temeke Marketndo mambingwa wawafunga bao 3-1 Kauzu FC leo jijini Dar
Kujiamini
kupindukia kumewaponza Kauzu FC baada ya kuchapwa kwa mabao 3-1 katika
mechi ya fainali na Temeke Market ambao wanakuwa mabingwa wapya wa
michuano ya Ndondo Cup.
Katika
mechi hiyo iliyochezwa leo kwenye dimba la Chuo cha Bandari maarufu
kama Wembley jijini Dar es Salaam, Kauzu waliingia uwanjani na kuanza
kucheza kama wana uhakika wa asilimia 100 kupata ushindi.
Lakini
baadaye makosa ya safu yake ya ulinzi ulianza kuwagharimu baada ya
Madebe kufunga bao la kwanza, Shabani Kisiga ‘Marlon’ akafunga la pili
kabla ya Adam Kingwade kumalizia la tatu.
Kauzu walifanikiwa kupata bao la la kufutia machozi katika kipindi cha kwanza katika dakika za nyongeza kupitia Rashid Gumbo.
Post a Comment