MTOTO WA KOFI OLOMIDE AKIMBIZA KWA FASHION
PARIS, Ufaransa
HUKU baba
yake, Koffi Olomide akiachiwa kwa dhamana baada ya kutakiwa kufungwa miezi 18 kwa kumpiga mnenguaji wake
Pame mwanamitindo anayechipukia, Didi Olomide ameanza kukimbiza katika fani ya mitindo
nchini Ufaransa hali inayomfanya kila mtu kumtabiria mazuri huko mbeleni.
Koffi
Olomide raia wa DR Congo, juzi kati alitimuliwa nchini Kenya alikokwenda kwenye
shoo kutokana na kusambaa kwa video iliyomuonyesha akimpiga teke dansa wake,
hivyo kutiwa jela kwa muda wa miezi 18.
Didi, 16,
ameonekana kuwa moto wa kuotea mbali kwa kuwa na umbo kali kiasi kwamba jarida
‘bab kubwa’ la Vogue liliamua kuzitumia picha zake na kuweka maneno ya kumsifia
kutokana na muonekano wake wa umbo, mavazi na nywele.
Watu wengi
wamekuwa wakimsifia katika mitandao ya kijamii hasa Instagram na kumtabiria
kwamba atakuwa tishio siku za usoni kwani kitendo cha kusifiwa na jarida hilo
kimemfanya kukubalika huku yeye mwenyewe akiwa na ndoto za kuwa mmoja wa
wanamitindo wanaosimamiwa na mwanamitindo Jean Paul Gaultier.
Post a Comment