MFANYABIASHARA ALIYEKUWA AKIJIINGIZIA MILIONI SABA KWA DAKIKA APANDISHWA TENA KIZIMBANI
Mfanyabiashara anayetuhumiwa kujiingia
fedha zipatazo shilingi milioni saba kwa dakika, Mohamed Mustafa Yusufali
amepandishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jijini Dar kusomewa
mashtaka yanayomkabili.
Yusufali na wenzake, wanakabiliwa na
mashtaka mbalimbali, yakiwemo udanganyifu, kughushi, kukweka kulipa kodi na
kutakatisha fedha haramu pamoja na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya
shilingi bilioni 15.6.
Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo
aliyefahamika kwa jina moja la Mashauri, ameiahirisha kesi hiyo mpaka Alhamisi
ya Julai 28, 2016, baada ya upande wa mashtaka kudaiwa kuwa na upungufu katika
hati ya mashtaka.
Post a Comment