Lionel Messi ahukumiwa kwenda jela miezi 21 kwa kukwepa kulipa kodi
Barcelona, Hispania
Mshambuliaji wa Argentina na
Barcelona, Lionel Messi amehukumiwa kifungo cha miezi 21 jela kutokana
na kulipa kukwepa kodi, vyombo vya habari vya Hispania vimeripoti.
Baba yake, Jorge Messi, pia amehukumiwa kifungo kwa kukwepa kulipa
kodi inayokadiriwa kufikia Euro 4.1 milioni kwa kipindi cha kuanzia 2007
hadi 2009.Hata hivyo, Messi mwenye tuzo tano za mchezaji bora wa dunia wa Fifa na baba yake wanaweza kukwepa maisha ya jela.
Kwa mujibu wa sheria za Hispania, kipengele cha kwenda jela chini ya miaka miwili kinaweza kutumikiwa kwa makubaliano maalumu.
Mshambuliaji huyo wa Barca na baba yake walikutwa na hatia ya makosa matatu katika kodi wakati wa hukumu ya jana katika Mahakama ya Barcelona.
Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, Lionel Messi alisema kwamba ‘hajui chochote’ juu ya usimamizi wa fedha zake, akidai kuwa kazi yake ni ‘kucheza mpira’.
TAZAMA VIDEO HAPA

Post a Comment