Uwoya amtia majaribuni Richie Mwezi Mtukufu jijini Dar
WAKATI Waislam wakiwa kwenye
Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya
juzikati alimtia majaribuni msanii mwenzake Single Mtambalike ‘Richie’
walipokuwa kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar kulikokuwa na
harusi ya mdogo wake Steve Mengere ‘Steve Nyerere’, Happy Mengere.
Irene Uwoya na Richie.
Kwenye ‘mnuso’ huo, Uwoya aliyekuwa
amevalia kivazi kilichoacha mapaja yake wazi, alionekana mara kadhaa
akimkumbatia Richie na hata paparazi wetu alipotaka kuwafutoa picha,
staa huyo alimshika kimahaba na kuwaacha watu wakinong’ona chinichini.
Single Mtambalike ‘Richie’
“Uwoya hivi haoni anamtia mwenzake
majaribuni? Na Mwezi Mtukufu huu analazimisha kupiga naye picha ya
kumkumbatia, ila hawa wasanii wamezoeana sana,” alisema mmoja wa
waalikwa aliyekuwa karibu na mastaa.
Paparazi wetu aliyekuwa eneo la tukio
alipojaribu kuwakaribia na kumuuliza Uwoya kulikoni anamfanyia mwenzake
vituko alisema, alijisahau kuwa Richie yupo kwenye Mwezi Mtukufu ila
alipiga picha hiyo kama pozi la kawaida tu na wala hakuwa na nia mbaya.

Post a Comment