Rais Magufuli Amuapisha Jaji Wa Mahakama Ya Rufani Pamoja Na Jaji Kiongozi, Pia Aagana Na Balozi Wa Oman Anayemaliza Muda Wake Hapa Nchini
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe
10 Juni, 2016 amemuapisha Mhe. Jaji Shaaban Ali Lila kuwa Jaji wa
Mahakama ya Rufani, Ikulu Jijini Dar es salaam.
Kabla ya kuteuliwa na kuapishwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Jaji Shaaban Ali Lila alikuwa Jaji Kiongozi.
Wakati huohuo, Rais Magufuli amemuapisha Mhe. Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali kuwa Jaji Kiongozi.
Kabla ya kuteuliwa na kuapishwa kuwa Jaji Kiongozi, Mhe. Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali alikuwa Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mkoani Tanga.
Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Leons Katipwa Wambali amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Jaji Shaaban Ali Lila ambaye amekua Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Katika hatua nyingine, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameagana na Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Saoud Ali Mohamed al Ruqaishi ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini.
Akizungumza na Balozi huyo, Ikulu Jijini Dar es salaam Rais Magufuli ameishukuru Oman kwa kuendeleza ushirikiano na uhusiano wa kihistoria na kidugu na Tanzania, na ameahidi kuwa serikali yake ya awamu ya tano ipo tayari kuongeza ushirikiano huo.
Mhe. Rais Magufuli pia amemuomba Balozi Saoud Ali Mohamed al Ruqaishi kufikisha salamu zake kwa Sultani wa Oman Mtukufu Qaboos bin Said al Said na kumueleza kuwa Tanzania inawakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara wa Oman na inatarajia kuona miradi ya ushirikiano katika uwekezaji ukiwemo mradi wa Bagamoyo inaanza kutekelezwa haraka.
"Naomba umfikishie salamu zangu za dhati Mtukufu Qaboos bin Said al Said, Sultan wa Oman na umwambie tunamkaribisha Tanzania na nitafurahi kuona mradi wa uwekezaji wa Bagamoyo unakuwa kielezo cha undugu na urafiki wetu uliodumu kwa miaka mingi" Amesema Rais Magufuli.
Tanzania kwa kushirikiana na nchi za Oman na China zimekubaliana kutekeleza mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
10 Juni, 2016.

wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha
Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali kuwa Jaji Kiongozi, Ikulu Jijini
Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza
Jaji Shaaban Ali Lila mara baada ya kumuapisha kuwa Jaji wa Mahakama ya
Rufani Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza
Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali mara baada ya kumuapisha kuwa Jaji
Kiongozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Shaaban Ali
Lila(kushoto) pamoja na Jaji Kiongozi Jaji Ferdinand Leons Katipwa
Wambali (kulia)mara baada ya tukio la uapisho lililofanyika Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Shaaban Ali
Lila(kushoto) pamoja na Jaji kiongozi Jaji Ferdinand Leons Katipwa
Wambali, wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji mkuu wa Tanzania Mohamed Chande
Othmani mara baada ya tukio la uapisho wa Majaji hao Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Shaaban Ali
Lila(kushoto) pamoja na Jaji kiongozi Jaji Ferdinand Leons Katipwa
Wambali, wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji mkuu wa Tanzania Mohamed Chande
Othmani pamoja na Majaji mbalimbali wa Mahakama Kuu na Mahakama ya
Rufani Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
kwa furaha huku akiwa amemshika mkono Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji
Shaaban Ali Lila huku viongozi wengine wakishuhudia ikulu jijini Dar es
Salaa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Balozi wa Oman hapa nchini Soud Al Ruqaishi ambaye anamaliza muda
wake wa kufanya kazi hapa nchini Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
Balozi wa Oman hapa nchini Soud Al Ruqaishi ambaye anamaliza muda wake
wa kufanyakazi hapa nchini.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Waandishi wa Habari waliofika Ikulu kwa ajili ya tukio
la uapisho wa Jaji wa Mahakama ya Rufani pamoja na Jaji Kiongozi Ikulu
jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU

Post a Comment