MZAMBIA MPYA WA YANGA APEWA JEZI YA COUTINHO
| CHIRWA |
SIKU
chache baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili ya kuichezea Yanga,
uongozi wa Yanga umemkabidhi jezi namba saba mshambuliaji wake Mzambia,
Obrey Chirwa.
Chirwa
alitua nchini wiki iliyopita akitokea FC Platinum ya Zimbabwe aliyokuwa
anaichezea pamoja na mshambuliaji tegemeo, Donald Ngoma.
Mzambia
huyo, alisaini kuichezea Yanga akichukua nafasi ya Mniger, Issoufou
Aboubacar aliyesitishiwa mkataba wake wa kuendelea kukipiga Jangwani
hivi karibuni.
![]() |
| COUTINHO |
Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh alisema jezi iliyobaki ni namba saba iliyokuwa inavaliwa na Mbrazili, Andrey Coutihno.
Saleh
alisema, jezi hiyo huenda akaanza kuonekana akiivaa mechi na Mazembe
itakayochezwa Jumanne ijayo mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
"Chirwa
tumempatia jezi namba saba iliyokuwa ikivaliwa na Coutinho, jezi ambayo
haina mtu kwa hivi sasa tangu ameondoka Mbrazili huyo.
"Hivyo
jezi ataanza kuonekana akiivaa kwa kuanzia mechi na Mazembe na nyingine
zote zitakazofuata za michuano ya kimataifa,"alisema Saleh.
Chirwa akiwa anaichezea Platinum, alikuwa anaivaa jezi namba 9 inayovaliwa hivi sasa na beki raia wa Togo, Vincent Bossou.

Post a Comment