Mfumo wa Kidigitali wa Kusoma Magazeti ‘M-Paper’ Wazinduliwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano na
Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (katikati) akiongea na
waandishi wa habari (hawapo pichani)wakati wa Uzinduzi wa Mfumo mpya wa
kidigitali wa M-Paper kwa kushirikiana na Smart Codes unaowezesha
wateja wa mtandao huo wanaotumia simu za Smartphone na kompyuta, kuweza
kusoma magazeti na majarida wayapendayo kwa gharama ya nusu bei ya
nakala halisi ya gazeti au jarida, Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha huduma
za ziada wa kampuni hiyo, Saurabh Jaiswal na Afisa Mtendaji Mkuu wa
Smart Codes, Edwin Bruno.
Mkuu
wa kitengo cha huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Saurabh
Jaiswal(kushoto)na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom
Tanzania,Rosalynn Mworia (kulia) wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa
Smart Codes, Edwin Bruno,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo
pichani) wakati wa Uzinduzi wa Mfumo mpya wa kidigitali wa M-Paper
unaotolewa na Vodacom Tanzania kwa ushirikiano wa Smart Codes
unaowezesha wateja wa mtandao huo wanaotumia simu za Smartphone na
kompyuta, kuweza kusoma magazeti na majarida wayapendayo kwa gharama ya
nusu bei ya nakala halisi ya gazeti au jarida.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Smart Codes, Edwin Bruno(katikati)akiwaelezea
waandishi wa habari jinsi ya kupakua bure program ya M-Paper kwenye
simu, Wakati wa uzinduzi wa Mfumo huo mpya wa kidigitali unaotolewa na
Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Smart Codes unaowezesha wateja wa
mtandao huo wanaotumia simu za Smartphone na kompyuta, kuweza kusoma
magazeti na majarida wayapendayo kwa gharama ya nusu bei ya nakala
halisi ya gazeti au jarida.Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha huduma za
ziada wa Vodacom Tanzania, Saurabh Jaiswal na Mkurugenzi wa Mawasiliano
na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Smart Codes, Edwin Bruno (kushoto) akiwaelezea
waandishi wa habari jinsi ya kupakua bure program ya M-Paper kwenye
simu, Wakati wa uzinduzi wa Mfumo huo mpya wa kidigitali unaotolewa na
Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Smart Codes unaowezesha wateja wa
mtandao huo wanaotumia simu za Smartphone na kompyuta,kuweza kusoma
magazeti na majarida wayapendayo kwa gharama ya nusu bei ya nakala
halisi ya gazeti au jarida.Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na
Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia.
Baadhi
ya wawakilishi wa vyomba mbalimbali vya habari vya magazeti wakiwa
kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa
Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (wasabi kushoto) pamoja na Afisa
Mtendaji Mkuu wa Smart Codes, Edwin Bruno(wasita kushoto)wakati wa
Uzinduzi wa Mfumo mpya wa kidigitali wa M-Paper unaotolewa na Vodacom
Tanzania kwa kushirikiana na Smart Codes unaowezesha wateja wa mtandao
huo wanaotumia simu za Smartphone na kompyuta, kuweza kusoma magazeti na
majarida wayapendayo kwa gharama ya nusu bei ya nakala halisi ya
gazeti au jarida.
Unaowezesha kupata habari za magazeti kupitia simu za Smartphone na kompyuta
Dar es
Salaam, Tuesday, June 21, 2016. Katika kutimiza dhamira yake ya
kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia leo
kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imezindua mfumo mpya wa
kidigitali wa M-Paper unaowezesha wateja wanaotumia simu za Smartphone,
na kompyuta kuweza kusoma magazeti na majarida wayapendayo kwa gharama
ya nusu bei ya nakala halisi ya gazeti au jarida.
Kwa kutumia mfumo
huu wa M-Paper. Vodacom imelenga kuwawezesha wateja wake kupata taarifa
zinazoandikwa kwenye magazeti na majarida wayapendao kwa urahisi kupitia
simu zao za mkononi. Programu inaotumika katika mfumo huu ambayo
imefanikishwa kwa ushirikiano wa kampuni ya kidigitali ya Smart Codes na
Vodacom inapatikana kwa kupakuliwa (download) bure katika tovuti ya http://mpaper.vodacom.co.tz/
Pamoja na wateja
kuweza kupakua bure programu hii, watakapokuwa wanahitaji kusoma
magazeti watalazimika kulipia nusu ya bei ya gharama ya nakala halisi
kwa gazeti atakalohitaji kusoma mteja, baada ya kupakua programu na
kuchagua gazeti alipendalo kuna maelekezo ya kulipia kabla ya kuanza
kusoma ambapo gharama za usomaji zinakatwa kwenye fedha ya muda wake wa
maongezi au kulipia kwa njia ya M-Pesa ambapo wasomaji waliopo nje ya
nchi wanaweza kulipia huduma hii kupitia kadi za kimataifa za kufanyia
mihamala ya malipo (Debit Card/Credit card)
“Vodacom Tanzania
kwa mara nyingine tumedhihirisha dhamira yetu ya kuwapeleka watanzania
katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia kwa kuanzisha huduma hii mpya
ya aina yake ya kuwawezesha watanzania kupata taarifa kupitia simu zao.
Huduma hii pia ni mwendelezo katika kurahisisha maisha kwa wananchi
ikiwemo kubadilisha maisha ya watu kwa kupanua wigo wa ajira nchini kama
ambavyo wabunifu wa programu hii wameweza kuitumia kurahisisha
maisha.”.Alisema Rosalynn Mworia,Afisa Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano na
Uhusiano wa Vodacom Tanzania.
Mworia alisema
tayari magazeti na majarida zaidi ya 52 yanapatikana katika programu hii
ambao wateja wanaweza kuanza kujisomea kwa gharama nafuu ya nusu bei ya
nakala halisi ambapo pia wanaweza kuchagua namna ya kulipia kupata
huduma hii ambapo mteja anaweza kulipia kwa wiki,kwa mwezi au kwa mwezi.
Kwa upande Afisa
Mtendaji Mkuu wa Smart Codes, Edwin Bruno alisema kuwa wameamua
kushirikiana na Vodacom kuleta huduma hii ya aina yake inaowezesha
watanzania kupata taarifa kwa urahisi na kwa gharama nafuu baada ya
kuona mtandao wa Vodacom umejipanga kuhakikisha wateja wake wanapata
huduma bora kwa kutumia ubunifu wa hali ya juu wa kiteknolojia kupitia
simu za mkononi.
“Hivi sasa tunaishi
katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia na teknolojia imekuwa
ikibadilika siku hadi siku ambapo hivi sasa mifumo mingi inayotumika ni
ya kidigitali,hivyo ushirikiano wetu na Vodacom katika kuanzisha
programu hii ya M-Paper na kuhakikisha inawafikia wateja wote wanaotumia
simu za SmartPhone ni ubunifu wa aina yake katika kuhakikisha taarifa
na habari zinawafikia wanajamii kwa njia rahisi na ya haraka na kwa
gharama nafuu.

Post a Comment