Kidoa: Nimemisi kutukanwa, kuvaa kihasara!

Video Queen mwenye figa matata, Asha
Salum ‘Kidoa’ amefunguka kuwa, ndani ya mwezi mtukufu amemisi kufanya na
kufanyiwa mambo kibao ikiwemo kuvaa nusu utupu na kutukanwa mitandaoni.
Kidoa aliitonya safu hii kuwa kabla ya
mwezi mtukufu alikuwa huru kupiga picha za mapozi na kuvaa anavyotaka
kisha kutupia mitandaoni lakini sasa hivi anabanwa kufanya hivyo.
“Ukiacha hilo la kuvaa mavazi yangu yale
niliyozoea, pia nimemisi kutukanwa, si unajua nilipokuwa nikitupia
picha hizo wapo watu waliokuwa wakinitukana. Huwa siogopi hilo, nimezoea
na ninaona ni kama sehemu ya maisha yangu,” alisema Kidoa.
Post a Comment