HII NDIYO SURA YA MWAMUZI MZAMBIA ALIYEPEWA RUNGU NA CAF AAMUE YANGA VS TP MAZEMBE PALE TAIFA
Mchezo
wa kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Young Africans ya
Dar es Salaam, Tanzania na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC), utachezeshwa na Mwamuzi Janny Sikazwe wa Zambia.
Sikazwe
atasaidiwa na Jarson Emiliano dos Santos kutoka Angola atayekuwa kwenye
mstari wa kulia (line 1) na Berhe O’Michael wa Eritrea atayekuwa upande
wa kushoto (line 2) huku Wellington Kaoma wa Zambia akiwa ni mwamuzi wa
akiba. Kamishna wa mchezo huo atakuwa Celestin Ntangungira wa Rwanda.
Pia mchezo huo utakuwa na Mratibu Mkuu Maalumu kutoka Msumbiji, Sidio
Jose Mugadza.

Post a Comment