HII HAPA ILE ISHU YA UONGOZI WA MTIBWA SUGAR KUITWANGA MKWARA SIMBA KUHUSU JEBA
| JEBA (KULIA)... |
Uongozi
wa Mtibwa Sugar umeionya Klabu ya Simba kuwa makini na suala la
kuwazungumzia au kufanya mazungumzo na wachezaji wake ambao wana
mikataba nao.
Mratibu
wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser amesema amekuwa akisikia Simba ina mpango
wa kuwasajili wachezaji watatu Shiza Kichuya, Ibrahim Rajab ‘Jeba’
na Ally Shomari. Lakini wana mkataba na Simba wanapaswa kuheshimu hilo.
“Kama
watakuwa wanazungumza wajue wanavunja kanuni na si sahihi, wakae nao
mbali na kama wanavutiwa nao basi waje tuzungumze nao,” alisema.
“Nimekuwa nikisikia tu kwenye vyombo vya habari, niseme tu kuwa nawakaribisha Simba waje.”
Kumekuwa na taarifa kwamba Simba ina mpango wa kuwasajili wachezaji hao katika harakati za kuimarisha kikosi chake.
Simba
iko katika mikakati ya kuimarisha kikosi chake kuhakikisha inarejea
katika heshima yake ikiwemo kushiriki michuano ya kimataifa.
Post a Comment