HANS POPPE ASEMA YANGA WAMEJITAKIA WENYEWE SUALA LA KESSY
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesisitiza, lazima
Yanga wapate barua kutoka Simba ili beki Hassan Kessy awe huru kucheza
Yanga.
Hans
Poppe amesema kipindi cha kuidhinisha usajili kwa Tanzania Bara
hakijawadia, hivyo lazima kuwe na barua ya ruhusa kutoka Simba ili Yanga
ianze kumtumia katika Kombe la Shirikisho.
“Yanga wao ni watu wabishi, wanajiona wako juu ya sheria. Hili lingeweza kwisha mapema kabisa, lakini hawakutaka kusikiliza.
“Tuliwaeleza
mapema hilo la Kessy, lakini waliona wanaweza kupita njia ya mkato.
Wanasema wao ni timu ya wananchi, ok,” alisema Hans Poppe.
Yanga
iliamua kutowatumia wachezaji wake wake akiwemo Kessy, Andrer Vicent,
Juma Mahadhi na Beno Kakolanya kwa kuwa haikuwa na uhakika kuhusiana na
suala hilo.
Hata
hivyo kumekuwa na kauli za kuchanganya, awali Caf ilisema ni lazima
kupata barua kutoka timu aliyotoka. Kauli ya pili kutoka kwa msemaji wa
shirikisho hilo ikaeleza wanaweza kuwatumia lakini lazima iwe makini
hasa kama kila kitu kipo kwenye msitari.
Lakini
katika mechi dhidi ya Mo Bejaia, Yanga iliamua kuchukua tahadhari kwa
kutomtumia Kessy na wenzake ili kuhakikisha inaondoa hofu hiyo.
Post a Comment