CAF YATANGAZA KUIFUTA ES SETIF LIGI YA MABINGWA AFRIKA, HII NI TAHADHARI KWA YANGA PIA
Shirikisho la Soka Afrika (Caf), limetangaza kuindoa ES Setif ya Algeria katika michuano ya Ligi ya Mabingwa.
Caf
imetangaza kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter, kuwa
Setif wameondolewa baada ya mashabiki wao kufanya vurugu katika mechi
dhidi ya Mamelodi Sundowns maarufu kama Masandawana.
Mashabiki
hao walianzisha vurugu kubwa na kusababisha mchezo huo kusimama kwa
kipindi kirefu, baadaye mwamuzi akalazimika kumaliza mpira wakati
mashabiki walipoamua kurusha mawe, chupa na vitu vingine uwanjani
wakionyesha kutofurahishwa kwa kuwa timu yao ilikuwa nyuma kwa mabao
2-0.
Huenda hilo linaweza kuwa funzo kwa mashabiki wa soka nchini hasa wale wa Yanga ambao timu yao inashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho, kwamba hawatakiwi kufanya vitendo vya kihuni kwa kuwa Caf, hawana mchezo katika hilo.

Katika
hatua ya makundi ES Setif ilikuwa ikitane na Zamalek katika mechi yake
ya pili iliyopangwa kupigwa Juni 29 jijini Cairo, Misri lakini sasa
safari imewakuta.

Post a Comment